Shirika linalochunguza nyendo za baharini limesema, maharamia wamevunja rekodi ya kuchukua mateka 1,181 mwaka 2010, licha ya kuongezeka kwa shughuli za kupiga doria katika bahari.
Shirika la kimataifa la mambo ya bahari (IMB) limesema meli 53 zimetekwa duniani ambapo 49 kutoka pwani ya Somalia na mabaharia wanane waliuawa.
IMB ameeleza kuwa ni jambo la "kutisha" kwa ongezeko la matukio ya kutekwa- idadi kubwa kutokea tangu shirika hilo lilipoanza shughuli za kufanya uchunguzi mwaka 1991.
Kwa ujumla, kulikuwa na mashambulio 445 ya uharamia mwaka jana- ongezeko la asilimia 10 tangu mwaka 2009.
Wiki iliyopita, utafiti tofauti uligundua kwamba uharamia unagaharimu uchumi wa dunia baina ya dola za kimarekani bilioni saba na 12 kwa mwaka.

Harakati 'zimedhoofishwa'

Pottengal Mukandan, mkuu wa kituo cha kuripoti uharamia cha IMB, " Takwimu hizi za idadi ya mateka na vyombo ni kubwa kuliko tulivyowahi kushuhudia."
Katika bahari huko Somalia, IMB, ilisema, maharamia wenye silaha nzito sana aghlabu huzishinda nguvu boti za wavuvi na baadae huzitumia kama msingi wa mashambulio zaidi.
Utekaji nyara 1,016 umefanywa na Wasomali kwa mwaka jana. Hadi sasa maharamia wa kisomali wameshikilia meli 31 huku kukiwa na zaidi ya mabaharia 700.
Licha ya meli zinazopiga doria, zilizozinduliwa mwaka 2009 kwenye ghuba ya Aden kupambana na mashambulio kadhaa, maharamia wa Somalia kwa sasa wanafanya shughuli zao mbali na bahari yao.