Bwana Gbagbo pichani ambaye anang'anga'nia kuitwa raisi wa Ivory Coast hivi sasa,ametoa kauli kwa raia wote nchini Ivory Coast kwamba kwa yeyote atakayethubutu kutoa hatua yake nje ya nyumba anayoishi atakiona cha mtema kuni.Alieleza hayo baada ya kuona kwamba wananchi wake wameamriwa na bwana Ouattara(mpinzani wake) kuanzisha maandamano kama yale ya Egypt na Tunisia.Mataifa mengine ulimwenguni pia hayamtambui kwamba bwana Gbagbo kama ni raisi wa nchini hiyo,kwani uchaguzi uliofanywa mwaka jana inaonyesha kuwa kiongozi wa chama pinzani  bwana Ouattara ndiye mshindi halali kwenye uchaguzi huo.
Pichani wafanyabiashara wa Cocoa nchini humo wakifunga magunia ya cocoa zao bila ya kuwa na uhakika wa kuuza biashara hiyo nje ya nchi kama ilivyo kawaida yao.Mataifa mbalimbali yameweka vikwazo vya kununua chochote toka Ivory Coast mpaka hapo bwana Gbagbo atakapojiondoa kwenye uraisi aliojipachika.HII NAYO KALI NYINGINE KWA AFRIKA,RAISI KAJIAPISHA MWENYEWE???NA HATAKI KUONDOKA HALI YA KUWA WANANCHI WAKE HAWAMTAKI..DUUH!!!AFRIKA KWELI BARA MOTO.