Uwanja wa Taifa (uwanja mpya) jana ulifurika watu ili mbaya katika ile harambee ya kuchangia waathirika wa janga la mabomu Gongolamboto.Timu mbili ziliundwa kwa ajili ya kuchangisha michango hiyo na timu zinyewe ni BONGO FLEVA na BONGO MOVIE,hapo wakati timu hizo zinaingia uwanjani.
 Ilikuwa siku ya furaha sana uwanjani hapo,ambapo kila msanii alijaribu kuonyesha kuwa sanaa aliyonayo sio moja na kwamba mambo ya kipira cha ndimu siku za nyuma aliyapitia,Pichani golikipa wa timu ya Bongo Fleva Tunda Man akijaribu kumpiga chenga msanii wa BONGO Movie JOTI huku umati wa watu ukiripuka kwa kelele za furaha uwanjani hapo.
 Mchezaji na msanii wa Bongo Fleva Ali Kiba akimtoka msanii na mchezaji wa Bongo Movie tayari kuweka majaro ili wakashinde.

Mshambuliaji wa timu ya Bongo Movie Ben Kinyaiya alipiga penalti nje na kuikosesha timu yake hata goli la kufuta machozi,mpaka mwisho wa mchezo Bongo Fleva 2-0 Bongo Movie.