Sikukuku ya kuzaliwa Mtume Muhammad s.a.w iliyofana sana katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam,wake kwa waume walihudhuria kwa wingi ukumbini hapo.
Kina mama nao walifika kwa wingi katika kusheherekea sikukuu hiyo ambayo hufanywa kila mwaka.Pichani chini makamu wa raisi akisalimiana na kila mmoja wakati akiingia ukumbini hapo.
Jumapili iliyopita katika ukumbi wa Karimjee jumuiya ya ISTIQAAM TANZANIA tawi la Dar es Salaam lilifanya shughuli maalumu ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume wa MUNGU MUHAMMAD S.A.W.Sherehe hizo zilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali toka kila kona ya Dunia,Pichani mwenye koti la kati ni makamu wa raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh: Bilal Mohammed Ghalib akiwa na Mashekh wakubwa wakisikiliza Mada zilizokuwa zikiendelea.
Kati ya Mashekh wakubwa waliohudhulia sherehe hizo mzee wa tatu kutoka kushoto mwenye kanzu rangi ya udongo ni mzee maarufu Ilala shariff shamba mzee Said Sleyyum akiwa makini kabisaa kufuatilia kwa ukaribu hotuba zilizokuwa zikizungumzwa.Mawaidha yalikuwa mazuri kwa kila aliyehudhuria sherehe hizo,Utaratibu huu ufanyika kila mwaka sehemu mbalimbali nchini. 
Hotuba zilizokuwa zikivutia watu waliohudhuria zilikuwa zikiendelea kwa kila aliyepata nafasi ya kutoa hotuba hizo.Hapa mmoja wa mashekh wakubwa nae alipata fulsa ya kutoa na kukumbusha yale mazuri aliyofundisha Mtume Muhammad S.AW.(Picha zote kwa hisani ya Said Sleyyum).