Kocha wa Simba, Mzambia Patrick Phiri, amesema kuwa kipa Juma Kaseja ataendelea kuwa chaguo lake la kwanza katika timu hiyo inayotetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara licha ya hivi karibuni kudaiwa kuwa kiwango chake kimeshuka.Pichani moja ya picha ya Juma kaseja akitunguliwa na mchezaji wa mabingwa wa soka Tanzania Yanga African.