Misururu mirefu imeonekana kwenye mabenki huko Ivory Coast huku kukiwa na wasiwasi wa mabenki kuporomoka baada ya benki ya Standard Chartered kusema kuwa inasitisha shughuli zake.
Ni benki ya nne kufungwa wiki hii kutokana na machafuko kufuatia uchaguzi wa Rais uliofanyika mwezi Novemba.
Awali iliripotiwa soko la hisa la Afrika Magharibi BRVM, lenye makao yake makuu Abidjan, imesitisha shughuli zake.

Wafanyakazi wa BRVM wameiambia BBC kuwa walikuwa wakifanya kazi, lakini haikufahamika wazi kama walikuwa wana uwezo wa kufanya malipo.
Tume ya uchaguzi inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ilimtaja Alassane Ouattara kuwa mshindi wa uchaguzi huo, lakini matokeo hayo yalibadilishwa na chombo cha kisheria na Bw Gbagbo anabaki madarakani licha ya kutishiwa kupewa vikwazo vya kimataifa na jeshi.