Rais wa Marekani Barack Obama amesema kiongozi huyo wa Libya aondoke madarakani na kuondoka nchini humo.(Pichani raisi Obama akitoa Order juu ya kuondoka kwa raisi Gaddafi).
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura - na kupita bila kupingwa - ya kuuwekea vikwazo utawala wa Muammar Gaddafi kutokana na hatua yake ya kutaka kuzima maandamano.Baraza hilo limeunga mkono kuweka vikwazo vya silaha na kupiga tanji amana, huku wakifikisha suala hilo katika Mahakama ya Kimataifa (ICC) kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinaadamu.(Pichani wajumbe wa UN wakipiga kura kuweka vikwazo kwa bwana Gaddafi).