KASHFA ya kukithiri kwa noti mpya bandia inazidi kuongezeka na sasa imebainika kuwa hata baadhi ya benki nchini zinashindwa kuzibaini na hivyo kujikuta zinaziingiza kwenye mzunguko.Wafanyakazi wa Benki wenyewe kuzitambua pesa feki nao ni kazi kwa upande wao.
Hali hiyo inatokana na Karani wa Fedha wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Februari 14 kuchukua fedha benki ya CRDB tawi la Lumumba na bila kutambua hatimaye akagundua amepewa noti nyingi za Sh 10,000 zikiwa bandia.
Hata pale mmoja wa wafanyakazi wa TSN aliyepewa noti hizo alipokwenda kuweka baadhi ya noti hizo kwenye moja ya benki bila kujua kuwa ni bandia, karani wa benki hiyo alizipokea na kuzipitisha kwenye mashine na kuridhika kuwa ni halali.
Ni kazi ya ziada kuzijua ipi Feki na Ipi Original,yani kama huna miwani kama muheshiwa hapo ujue umeingizwa mjini.Tahadhari sana kabla ya kutoa na kupokea pesa ikague mara mbili mbili na hata kama unahisi kuna utata jaribu kumuuliza yoyote ili kuepuka kujiweka katika hali ngumu.
0 Comments