Kauli iliyotolewa bungeni mjini Dodoma na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuwa hakuna ukiukwaji wowote wa sheria katika uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha, imewatibua nyongo madiwani 14 wa Chadema ambao wameamua kususia uchaguzi wa kamati za kudumu na wenyeviti wa kamati za halmashauri.
Madiwani hao walisusia kikao hicho kilichofanyika jana mara baada ya kusikia tamko la Pinda bungeni wakati akijibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa wabunge.
Akizungumza na waandishi wa habari, Msemaji wa Chadema Zebedayo Bayo, alisema jana asubuhi walikutana katika kikao cha pamoja na madiwani kutafuta muafaka.
Alisema kabla ya kufikia makubalioano walisikia tamko la Waziri Mkuu kuwa hivyo kutibua mambo.
“Jana tulikutana na kuwaomba wataalamu watoke katika kikao na kuanza kuzungumza na sisi madiwani wa pande zote kwa lengo la kumaliza mgogoro lakini baadaye zikaja taarifa kuwa serikali imetoa tamko hilo ambalo sisi hatulikubali,”alisema
Alisema kauli ya Pinda kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa hakina kwamba kama kuna wenye malalamiko waende mahakamani si cha kiungwana na chama hicho kitaionyesha dunia kuwa hatukubaliani na kauli hiyo.
“Tumeshtushwa na kauli ya Waziri Mkuu wakati akijibu maswali ya papo kwa papo tunaipinga na tutaendelea kusema uchaguzi ule wa Meya ulikuwa batili,” alisema.
Alieleza kuwa Waziri Mkuu alipaswa kuita pande zote na kusikiliza hoja zao na kutoa uamuzi ambao ungewaridhisha kuwa ana nia njema ya kuendeleza demkrasia na utawala bora. Akizungumzia tukio hilo Meya wa Jiji la Arusha, Gaudence Lyimo, alisema kuwa wamesikitishwa na kitendo cha madiwani wa Chadema kuamua kutoka ndani ya kikao hicho.
0 Comments