Mjumbe wa Bodi ya Mradi wa Maji Safi na Afya Bora Ifakara (MSABI), Honorati Urassa (kulia) akimshukuru Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu kwa msaada wa Sh milioni 35 zilizotolewa na TBL kwa ajili ya kufanikisha mradi wa ujenzi wa visima 10 vya kisasa kwenye shule 10 wilayani Kilombero, mkoani Morogoro.