Chama cha Wananchi (CUF), kimesema kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne kila mwaka, ni kielelezo cha hali duni ya elimu nchini inayotokana na ubishi na upogo wa serikali kutotaka kushirikiana na wadau wa elimu na vyama vya siasa.
Kauli hiyo ya CUF ilitolewa na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wake Tanzania Bara, Julius Mtatiro alipozungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana.