Waziri wa mambo ya ndani ya Italia bwana Roberto Maroni ameonya wakimbizi wote toka Tunisia kutojaribu kufanya aina yoyote ya uharifu.Akizungumza na waandishi wa habari amesema zaidi ya wakimbizi 5000 toka Tunisia wameripotiwa kuingia nchini Italia.Alisisitiza kuwa anahofia sana makundi yanayojitoa muanga ya Al Qaida kufanya matukio aina yoyote mabaya nchini humo.
0 Comments