Gattuso anayechezea klabu ya Ac Milan pia timu ya taifa ya Italia, alizozana na Joe Jordan mwenye umri wa miaka 59 na baadae akamsukuma shingoni.
Hapa anaonekana akitaka kupiga kibao kwa jinsi alivyopandwa na hasira.Kwa heshima zetu waafrika huwezi kuzozana na mtu mzima aliyekuzidi umri kama huyu,kwa wenzetu ni hali ya kawaida kutokana na malezi waliyokuwa nayo.
 Ona jinsi alivyomkosea adabu kocha huyu,baada ya kuona hafanywi lolote alimkaba kabisaaa.

 Baada ya mechi kumalizika alikwenda kwenye benchi la timu ya Arsenal akaanzisha ugomvi na wachezaji wa Arsenal,hata hivyo alidhitiwa vilivyo kiasi akatulia.
Inaelekea huyu jamaa ana fani zaidi ya mpira,kwani ugomvi anaupenda sana,kama ujioneavyo aliendea kubishana na kusukumana na wachezaji wa Arsenal..Imethibitishwa kuwa rasmi mchezajia Gatuso ameona msamaha kwa kile kitendo chake cha kumvunjia heshima Kocha Joe Jordan,alidai kwamba alishindwa kujikotroo kutokana na hasira alizokuwa nazo,chama cha mpira duniani FIFA kimesema kinamjadili na kitatoa maamuzi juu ya Gatuso hivi karibuni.