Ukifika Zanzibar ulizia sehemu moja maarufu inaitwa Forodhani,chakula kipendwacho na wengi pale ni Urojo,kama wewe ni Mnyamwezi wa Nzega kama mie hushibi Urojo huo... basi agiza mikate maarafu ili uupige na chai  waitwa mkate wa BOFULO au Boflo yani huu mkate unapoununua wa moto ni mzuri saana,ila ukishakaa sana na kupigwa na upepoo mmh shughuli unayo.Pichani ni mikate ya Boflo ikiwa tayari kwa mauzo.