Kama tulivyoona hapo nyuma malezi ya watoto si jambo rahisi,lakini linapokuja suala la malezi ya watoto(sisi wazazi wa kiafrika) hapa ulaya huwa ni kazi nyingine kabisa.(Ni ngumu kuliko afrika) Na sababu ni hizo ambazo nimejaribu kuzibainisha katika mada yetu sehemu ya kwanza.Leo nitajaribu kuiendeleza mada yetu kwa mifano iliyo hai ambayo imetokea kwa jamaa zangu wa karibu.
Watoto wengi huwa wanakimbia kutoka kwa wazazi wao wanapofikia umri wa balehe yaani kuanzia umri wa miaka kumi na sita mpaka ishirini na moja,Na sababu kubwa ni mtoto kuona hapewi uhuru anaoutaka kama wanavyopewa watoto wa kizungu.Kuna kijana mmoja ambaye aliamua kuondoka kwao na kwenda kukaa kwa mpenzi wake wa kike(kwa wazazi wa mpenzi wake) kwa sababu mzazi wake alikuwa anamdhibiti juu ya tabia mbaya ambazo alikuwa anaifanya huyu kijana kama vile uvutaji wa sigara na bangi,kuwa na marafiki wasioeleweka,kurudi nyumbani nyakati mbaya za usiku na kumuepusha na uwezekano wa kufanyika zinaa nyumbani kwake.(kumzuia asiingie na mwanamke wake chumba cha kulala).
kwa upande mwingine yule mtoto alipokelewa vyema upande wa pili(kwa wazazi wa msichana) kwani wao hawaoni tatizo lolote kwa watoto wao kufanya kile wanachokitaka ili mradi mtoto wao anaenda shule na ana furahiaa maisha,hata mzazi wa mtoto wa kiume alipoenda kulalamika kwa mzazi mwenzie aliambiwa kwamba hilo sio shauri lao.Hii yote imetokana na mtoto kutopewa mafunzo yanayotakiwa toka zamani na kutegmea aongoke akiwa mkubwa.Matokeo yake mtoto akaishia kwenye madawa ya kulevya na akashindwa na masomo kiasi cha sasa ameshakuwa mkubwa hajui pa kuanzia na madeni yamemjaa kibao na kuwa black listed.
Kuna watoto wengi wa kike ambao wamepiga picha za uchi na matokeo yake picha kusambaa katika mitandao kitendo ambacho kinawafedhehesha wazazi kiasi ambacho wazazi wanatamani kuikimbia hata nchi kwa aibu.
-Mada itaendelea wiki ijayo,
-kwa wenye maoni,mswali na ushauri msisite kutuandikia kwa email yetu,magangaone@gmail.com au kwa simu namba +32 49 222 33 25,Ahsanteni.
0 Comments