Jamuhuri ya Democrasia ya Congo ni nchini mojawapo ambayo kwa ukubwa naifananisha na jimbo la Mississippi nchini Marekani.nchi iliyojaaliwa kila aina ya maliasilia,wakongo wana ardhi yenye rutuba nzuri sana,wana maeneo makubwa sana kwa kilimo,Hali ya hewa nchini Congo kwa kweli inavutia sana.ndio nchi pekee duniani yenye kutoa madini yanayotumika kwenye mawasiliano ya simu za mikononi,huwezi kupata madini hayo nchi yoyote duniani.Ina machimbo mengi sana ya dhahabu na mengine meengi sana ya kujivunia kama wakongo,cha kushangaza nchini Congo ni kwamba huwezi kupata matatibabu kirahisi kutokana na ukame wa madawa,huwezi kupata elimu bora kutokana na ukosefu wa shule za kutosha,hali ya umeme ndio kabisa inatisha nchini humo,pamoja na utajiri wa maliasilia zoote walizonazo Congo ipo katika nchi masikini duniani.