Andrew Ryan mwenye umri wa miaka 32 aliiba msahafu toka kwenye maktaba ya mji wa Cumbria na kisha kwenda katikati ya mji na kuuchoma moto msahafu huo kwenye eneo ambalo kulikuwa na maduka mengi. Andrew alilifanya tukio hilo mwezi januari mwaka huu akidai analipiza kisasi kwa vitendo wanavyofanyiwa wanajeshi wa Uingereza nchini Afghanistan. Andrew ambaye ana historia ya kufikishwa mahakamani mara sita kwa makosa tofauti tofauti likiwemo kosa la kutoa kauli za ubaguzi wa rangi kwenye mechi ya soka, alihukumiwa kwenda jela siku 70. Akitoa hukumu ya kesi hiyo, jaji Gerald Chalk alimwabia Andrew: "Wewe ni mtu mwenye historia ya kufanya matukio ya uhalifu na kuvunja sheria". "Uliamua kufanya kosa hili kubwa na kuwavunjia heshima waislamu", alisema jaji Chalk. Andrew aliambiwa kuwa anaruhusiwa kuonyesha hisia zake hadharani lakini si kwa kufanya kitendo ambacho kitasababisha ukosefu wa amani kwenye jamii. Andrew alikiri kosa la kufanya kitendo cha kueneza chuki za dini na pia alikiri kufanya wizi kwa kuiba msahafu toka kwenye maktaba ya manispaa. | ||
(Habari kamili na Nifahamishe) | ||
0 Comments