Bidada Zainab akiwa amepozi kwenye kiti na mama yake mzazi Innocent nyuma yake wakipata Flash kama kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa bidada Zainab,Zainab alitimiza miaka 14 hivi karibuni na kufanya bonge la party nyumbani kwao na kujumuika na watu wengi waliohudhuria tafrija yake.
Kwenye party hapakuwa na watoto tu bali na watu wazima walimpa sapoti ya nguvu bidada Zainab kama ujioneavyo pichani.
Bwana Ally na dada yake hawakubaki nyuma pale walipopiga viwalo vya nguvu ili kujumuika kwenye tafrija ya bidada Zainab.
Kamanda langu,kaka yangu Yahya F.Mbogo Mnyamwezi wa ukweli akiwa na mkewe ambaye ni shemeji langu la nguvu bi Aysher na watoto wangu kama mnavyowaona wakipata Flash ili kuweka kumbukumbu ndani ya party ya Zainab iliyofanyika nchini Uingereza hivi karibuni.
Mke wa kaka (shemeji yangu) bi Aysher akiwa amepozi na katoto ka kaka akisubiri kuletewa nyama choma kwenye party ya bidada Zainab.
Kama kawaida baada ya party ni mambo ya Flash,hapo shemeji yangu akipata Flash,ilikua party nzuri iliyofangasha mamia ya wakazi waliompenda bidada Zainab.Maganga One Blog inapongeza sana bidada Zainab kwa kusheherekea miaka 14 yake ya kuzaliwa na kumsisitiza apige book kwa sana,elimu ndio mambo yote kwa dunia ya sasa.
0 Comments