Shambulio la bomu katika eneo kuu la wazi kwenye mji wa Marrakesh nchini Morocco umeua takriban watu 14 na kujeruhi 20, wengine wakiwa raia wa kigeni.
Mlipuko huo ulipasua mgahawa wa Argana kwenye eneo la wazi la Djemaa el-Fna, eneo maarufu kwa watalii.
Wizara ya mambo ya ndani imesema ushahidi kwa sasa unaelekea kuwa ni shambulio la bomu baada ya ripoti za awali kupendekeza kuwa ni mlipuko wa gesi.
Morocco imeshuhudia maandamano kwa muda wa miezi miwili dhidi ya mfalme Mohammed V1 huku kukiwa na wimbi la ghasia katika eneo hilo.
Shambulio la mwisho la kigaidi Morocco lilitokea mwaka 2003 katika mji wa Casablanca- watu 45, wakiwemo watu waliojitoa mhanga, waliuawa.