Majeshi yanayompinga kiongozi aliyekataa kuondoka madadarakani Laurent Gbagbo, wamefanya shambulio la mwisho katika kasri ya rais ambapo amejificha.Bw Gbagbo amekuwa katika mazungumzo na Umoja wa Mataifa kuhusu mipango ya kuondoka kwake, baada ya kuzungukwa na majeshi yanayomtii hasimu wake Alassane Ouattara.
Chanzo kutoka serikali ya Ufaransa kimesema milio ya risasi ilisikika nyumbani kwa Bw Gbagbo mjini Abidjan.
Lakini tume ya uchaguzi wa Ivory Coast ilimtangaza Bw Ouattara kuwa mshindi, matokeo ambayo yaliungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
Bw Gbagbo na familia yake wanaaminika kuwa wamejificha katika handaki ndani ya kasri ya rais, ambayo ilikuwa ikidhibitiwa na majeshi yake.
Siku mbili za mapigano zilimalizika siku ya Jumanne na majadiliano na Bw Gbagbo yaliendelea hadi usiku wa manane.
Lakini siku ya Jumatano asubuhi ilionekana majeshi ya Ouattara yalishindwa kuvumilia.
"Tutamtoa Laurent Gbagbo kutoka mafochoni na kumkabidhi kwa rais wa Jamhuri" amesema Sidiki Konate, msemaji wa waziri mkuu wa Bw Ouattara, Guillaume Soro.
0 Comments