Majeshi yanayomtii Rais wa Ivory Coast anayeungwa mkono na Umoja wa Mataifa, Alassane Ouattara, yanaonekana kuwa katika hatua ya mwisho ya kumwondoa mpinzani wake, Laurent Gbagbo, ambaye amekataa kuachia madaraka.

Katika mji mkuu, Abidjan, majeshi yanayomwuunga mkono Ouattara yameanza mashambulio kwenye makazi ya Rais yenye ulinzi mkali.
Majeshi ya Ufaransa yamewapeleka takriban raia wa kigeni 500 kwenye kambi ya jeshi kutokana na usalama kuzidi kuyumba mjini humo.
Majeshi yanayomwuunga mkono Ouattara yalianzsiha mapigano mapya siku ya Jumatatu.
Mwandishi wa BBC John James aliyopo katikati ya mji wa Bouake alisema hii inaonekana ni dakika za majeruhi kwa serikali ya Laurent Gbagbo.
Mkazi wa Abidjan alisema mapigano yalikuwa yakipamba moto katika wilaya ya Cocody kaskazini mwa nchi hiyo, eneo yalipo makazi ya Rais huyo.