Majeshi yanayomtii Rais wa Ivory Coast anayetambuliwa na jumuiya za kimataifa , Alassane Ouattara, yamezingira mji mkuu wa Abidjan kutoka maeneo mbalimbali
Awali mkuu wa majeshi wa Bw Gbagbo aliomba hifadhi kwa balozi wa Afrika Kusini.Umoja wa Mataifa umesema Bw Gbagbo alishindwa kwenye uchaguzi mwaka jana, lakini amekataa kukabidhi madaraka kwa Bw Ouattara.
Majeshi yanayomwuunga mkono Bw Gbagbo yamekuwa yakishika doria kwenye wilaya za mji huo, na kuweka vizuizi vya barabarani.
Mwandishi wa BBC Valerie Bony mjini Abidjan alisema kumekuwa na mapigano makali kwenye kituo cha televisheni cha taifa liliopo eneo wanalokaa wakazi, na milipuko kwenye vitongoji kaskazini mwa nchi hiyo.
0 Comments