Katika kampeni za uchaguzi ambao ulimalizika mwishoni mwaka jana,Mbunge Highness Samson Kiwia aliwahaidi wananchi katika jimbo lake kuwa atawasaidia gari la kubeba wagonjwa ambalo litawasaidia wananchi kuwasafirisha hadi katika hospitali zingine na baadhi yao kuwatoa majumbani kwao hadi katika zahanati hiyo ahadi ambayo ameitekeleza ndani ya siku 90 kama alivyoahidi.Pichani akilikabidhi gari hilo kwa mganga mkuu wa hospitalini hapo Bernad Straton.
Katika hali ambayo hakuitaraji muheshimiwa Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi,alilazimishwa na wananchi wa mkoa wa Mwanza kuimba nyimbo zake ambazo zilikuwa zinapendwa siku za nyuma mpaka leo ilibidi aingie mzigoni na kuanza kuimba kama unavyomuona pichani.Mr Sugu kama watu wanavyopenda kumuita Mbunge huyo alikonga nyoyo za wapenzi wa Mwanza katika kile kusema anapendwa na vijana wengi anapoimba nyimbo zake.(Picha zote kwa hisani ya Gsengo).
0 Comments