Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni.
Taasisi ya World Vision nchini imetoa msaada wa dawa kwa ajili ya kupunguza magonjwa ya minyoo na kichocho kwa wanafunzi wa shule za msingi.
Mkurugenzi Msaidizi wa taasisi hiyo, Anatoli Rugaimukamu, alisema wametoa msaada huo kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye magonjwa hayo kwani yamesahaulika na kutopewa kipaumbele.
“World Vision imetoa msaada wa madawa kwa ajili ya kuwasaidia watoto kwa kuwa ni magonjwa yenye madhara makubwa na yalikuwa yamesahaulika kupewa kipaumbele,” alisema Rugaimukamu.
Akipokea msaada huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni, alisema magonjwa hayo yanayowapata watoto wengi hasa walioko shule za msingi na yalikuwa hayapewi kipaumbele.
“Wizara ya Afya inaishukuru taasisi ya World Vision kwa kutoa msaada huo kwa kuwa tunaamini itaweza kuwasaidia wanafunzi wa shule za msingi hasa wale waliokuwa na matatizo hayo,” alisema Nyoni. Nyoni alisema kuwa mikoa ambayo inaongoza kwa watoto wenye magonjwa hayo ni Dodoma, Manyara, Singida, Rukwa na Tabora.
0 Comments