KICHWA cha ukweli kinachosumbua katika Muziki wa Bongo Fleva, Mwasiti Almas (pichani) ameibuka na kutoa yake ya moyoni kuwa anahitaji mume wa kumuoa.
Katika mahojiano na kona hivi juzijuzi, jijini Dar es Salaam, Mwasiti ambaye anasumbua vilivyo na kibao cha Siyo Kisa Pombe, alisema anamhitaji mwanaume huyo baada ya mwaka mmoja
“Niliamua kukaa miaka miwili bila mpenzi maana sikutaka usumbufu, lakini kubwa zaidi nilikuwa naweka mipango yangu ya fedha vizuri. Kiukweli naweza kusema sasa nahitaji mwanaume wa kunioa na siyo ‘boyfriend’ ila nitavuta subira hadi baada ya mwaka mmoja,” alisema Mwasiti.
Mwasiti ni zao la Taasisi ya Jumba la Vipaji Tanzania (THT), ambaye ngoma yake ya Hao aliyoisimamisha na mkali Chid Benz ilimuweka vizuri kwenye ramani ya muziki wa Kizazi Kipya.(Habari toka Bongflava).
0 Comments