Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete akipungia mkono wananchi waliofurika uwanja wa Amani mjini Zanzibar hiyo jana katika maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Muungano 26/4/2011.
Alipanda juu ya jukwaa na kukutana na mwenyeji wake rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein,hapo walikuwa wakisalimiana na kupongezana kwa kuhadhimisha miaka 47 ya Muungano.
Rais Jk alipata fulsa ya kuwasalimia wake wa marais wastaafu wa Zanzibar.
Kama ilivyoada rais kukagua gwaride,Rais Jakaya Kikwete akilikagua jeshi la kujenga taifa,kwa kweli hali ya hapo uwanjani Amani ilipendeza sana hapo jana.
0 Comments