Jana jioni kwenye ufukwe wa bahari sehemu za Blankenberge nchini Belgium kijana mdogo wa umri wa miaka 5 alikimbizwa hospital baada ya kugongwa na tram.Kijana huyo ambaye alikatiza ghafla na kufanya dereva wa tram hiyo kushindwa kumuona na kumgonga,hali ya mtoto huyo ni mbaya sana kutoka na ajali hiyo.Dereva wa tram hiyo alishindwa kuendesha tena tram ile kutokana na kupigwa na butwaa na kushindwa kujua nini afanye,Dereva huyo yupo chini ya madaktari wa akili ili kumuhudumia kutokana na msongo wa mawazo alionao dereva huyo.