Bado natafakari juu ya siasa ya nchi yetu,kwenye kampeni malumbano na maneno ya ajabuajabu ila pale wanapokutana bwanaaa ebu jionee mwenyewe...Ila napenda sana hatuna uhasama wala kununiana kama nchi nyingine,hii kweli Demokrasia ya ukweli.
Nimegundua kuwa siasa sio chuki wala ugomvi,yani kama tutaendelea hivi kama ujioneavyo pichani basi tutadumu na Amani yetu milele, na nchi zenye kupenda kupigana zitabaki kutuona wajinga kwa uoga wetu kumbe wao ndio wajinga kwa kuuana kisa siasa.Siasa ni malumbano yenye kuleta maendeleo,siasa ni kukumbushana kwa kupingana bila kuleteana mikwaruzo.siasa ina tafsiri nyingi sana huu ni mtazamo wangu tu.
0 Comments