Watu waliojenga katika Bonde la Msimbazi, kuanzia Salender Bridge, Muhimbili, Jangwani hadi Vingunguti, wametakiwa kuondoka mara moja katika eneo hilo na kwenda kutafuta maeneo mengine ya kuishi kabla serikali haijatumia dola kuwaondoa kwa nguvu.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, alipozungumza jana.
Alisema serikali ina mpango kabambe wa kulifanya Bonde lote la Msimbazi kuwa eneo kuu la wazi (centre park) la Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya matumizi ya michezo, hivyo hakuna anayeruhusiwa kuishi hapo hata kama ana hati. “Kwa hiyo, wote walioko katika Bonde la Msimbazi, kuanzia Salender Bridge, Muhimbili, Jangwani hadi Vingunguti wakae chonjo, watafute maeneo mengine. Hata kama wamepewa kihalali haisaidii kitu. Bonde la Msimbazi siyo kijiji,” alisema Profesa Tibaijuka.
Alisema tayari Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imeshaagizwa na wizara kutekeleza mara moja agizo la Rais Jakaya Kikwete la kutaka mabati yaliyezungushiwa katika viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam yabomolewe mara moja.
Mbali na mabati hayo, Waziri Tibaijuka alisema pia kuna mtu, ambaye ameligeuza eneo la viwanja vya Jangwani kuwa sehemu ya kumwaga kifusi bila kujua kwamba, kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Alisema tamko rasmi kuhusu suala hilo litatolewa na serikali wakati wowote, kuanzia sasa.(source Nipashe).

Maeneo haya hufanywa dampo ya kutupia takataka wakati ni karibu kabisa na makazi ya watu,hali hii ni hatari hasa panapotokea milipuko ya magonjwa.Uchafu huu uzuia maji kwenda mahala husika na kufanya harufu mbaya sana ukipita karibu na maeneo hayoo.