Bei ya chakula katika masoko ya jijini Dar es Salaam, imeanza kushuka kutokana na nafaka yakiwemo mahindi kuanza kuingia kwa wingi kutoka mikoa ya Dodoma, Mbeya na Rukwa. |
Mwarami alisema mwezi uliopita kilo ya mahindi ilikuwa ni kati ya Sh. 480 na 500 lakini mwezi huu imeshuka na kufikia kati ya Sh. 420 na 450.
Kwa upande wa maharage alisema mwezi uliopita yalikuwa yakiuzwa kati ya Sh. 1,550 ma 1,600.
Kuhusu mahindi kutoka ghala la serikali ambayo wafanyabiashara waliagizwa kuuziwa kwa Sh. 380 kwa kilo na kuuza kwa wananchi kwa Sh. 500, alisema gharama za uzalishaji ni kubwa tofauti na maagizo ya serikali.
Alisema masharti yaliyotolewa na serikali yamekwamisha wafanyabiashara wengi kwenda kununua mahindi hayo ambapo kwa sasa bidhaa hiyo inaingia kwa wingi kutoka mikoani na bei yake ni nafuu inayowapa faida.
"Bei ya uzalishaji ni kubwa hivyo serikali ingekaa chini na sisi ikafahamu gharama tunazotumia ndipo itoe masharti hayo...lakini sijui kama yatapata soko tena kwani mahindi mapya yanaingia kwa kasi hapa sokoni kutoka mikoani," alisema Mwarami.
Naye Mwenyekiti wa soko hilo, Sultani Kijumbo, alisema bei ya chakula imeshuka kutokana mazao kuanza kuingia kwa wingi sokoni hivyo hali ya maisha itabadilika. Kijumbo alisema soko hilo halikupata fursa ya kununua mahindi kutoka katika ghala la serikali kwa kuwa zoezi hilo lilikabidhiwa chini ya wafanyabiashara wenye mashine za matayarisho ya unga.
CHANZO: NIPASHE
0 Comments