Suzanne Mubarak atazuiliwa katika gereza moja mjini Cairo, shirika la habari la Mena limesema.
Bi Mubarak, 70, na mume wake wamehojiwa kuhusiana na tuhuma za "upataji mali kinyume cha sheria".
Rais Mubarak, ambaye alikaa madarakani kwa miaka 30, aliondoka madarakani mwezi Februari baada ya wiki kadhaa za maandamano.
Rais huyo wa zamani anashikiliwa na mamlaka za nchi hiyo zinazohusiana ma upatikanaji wa mali kintyume cha sheria, kwa mashitaka ya kutumia vibaya madaraka yake na kujipatia utajiri. Pia anatuhumiwa kwa kuhusika na mauaji ya watu waliokuwa wakipinga utawala wake.
Bw Mubarak, 80, kwa sasa yuko hospitali katika mji uliopo kwenye mwambao wa bahari ya Sham wa Sharm el-Sheikh, baada ya kupata matatizo ya moyo.
Baraza la kijeshi ambalo limeingia madarakani tangu Bw Mubarak aondoke, limeahidi kuwafikisha mahakamani wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi.
0 Comments