Kiongozi wa upinzani wa Uganda, Kiiza Besigye, anasema ataendelea kufanya maandamano ingawa alishambuliwa na kujeruhiwa na polisi.
Bwana Besigye alisema hayo hospitali mjini Nairobi, Kenya, ambako amekuwa akitibiwa baada ya kurushiwa pili pili machoni.
Madaktari wanasema ameumia vibaya machoni lakini hali yake inatengenea
Shirika la kupigania haki za kibinaadamu la Umoja wa Mataifa linaitaka Uganda kuacha kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji.(source bbc)