Mchezaji wa Manchester United Michael Owen akiwa amewekwa chini ndani ya eneo la hatari na mchezaji wa Arsenal Gael Clichy wa pili kulia,ila mchezesha mpira alikataa kuwapa Manchester penati na kusema mpira uendelee.
Alex Song wa Arsenal kulia(17) akimzuia mchezaji wa Manchester United Wayne Rooney(10) asifurukute na kuleta madhara langoni mwa timu yake.
Wayne Rooney akiwa ameshika kiuno aamini kile kilichotokea baada ya Aaron Ramsey kuandika bao la .  kuongoza kwa timu yake ya Arsenal,na mpaka mwisho wa mchezo mmmh Manchester United 0 - 1 Arsenal
Mlinda mlango wa timu ya Manchester United akiruka bila mafanikio yoyote baada ya mchezaji wa Arsenal Aaron Ramsey kuiunganisha krosi na kuandika goli la ushindi,pichani beki wa Manchester Fabio mwenye jezi nyeusi akiangalia jinsi mpira ulivyokuwa ukimalizia kutingisha nyavu zao,mpaka mwisho wa mpira Arseanal walitoka uwanjani washindi wa goli 1 - O.