Mwanzilishi na kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaeda Osama Bin Laden ameuwawa na majeshi ya Marekani nchini Pakistan, rais Obama amesema.
Kiongozi huyo wa al-qaeda aliuwawa katika operesheni ya ardhini nje ya mji wa Islamabad kwa mujibu wa taarifa za kijasusi.
Bw Obama amasema baada ya ufyatulianaji wa risasi, majeshi ya Marekani ilichukua mwili wake.
Bin Laden anashutumiwa kwa kuhusika katika baadhi ya vitendo vya ukatili ikiwemo mashambulizi mjini New York na Washington, mnamo Septemba 11, 2001.
Kifo chake ni pigo kubwa kwa kundi la al-qaeda lakini kuelezea hofu kuwa huenda wakashambuliwa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi.
Bw Obama anasema alielezea Agosti, mwaka uliopita, kuhusu kule Osama Bin Laden amejifisha. Kufuatia uchunguzi wa ujasusi waligundua amejificha mjini Pakistan.

Wiki iliyopita rais Obama alitoa amri kwa operesheni kufanyika ''kumsaka Bin Laden'' . Bw Obama amesema operesheni hiyo iliendeshwa na kundi ndogo la wanajeshi wa Marekani katika eneo la Abbottabad, Kaskazini mwa Islamabad.
''Baada ya ufyatulianaji wa risasi, Bin Laden aliuwawa na mwili wale kuchukuliwa na majeshi ya Marekani'' rais Barack Obama amesema.