Baadhi ya watu wamekuwa wakipigwa risasi hovyo na wanajeshi nchi Ivory Coast,pamoja na kukamatwa kwa aliyeng'ang'ania madaraka nchini humo bwana Gbagbo ila hali bado ni tete nchini humo.
Ebu ona jinsi huyu mwanjeshi anavyowinda wenzake,yani hapo mtu akitokeza tu ankula risasi.
Na huyu mwingine hapa akiwa makini kabisa kwa kumsubiri atakayetokea tu ammalize,kwa kweli nchini Ivory Coast panatisha kwa mauaji.
Mmoja wa wanajeshi wa rais wa sasa akiwa amepoteza maisha baada ya kugongwa na gari na waasi wa bwana Gbagbo.
Duuh wanyonge hawana haki kabisaa,hapa raia wema wakiwa chini ya ulinzi na kupelekwa kusikojulikana kwa mateso.
Mabomu yanayoendelea kulipuliwa yanaiweka nchi ya Ivory coast katika wakati mgumu sana kwa wakazi na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Kama unavyojionea maiti zikiwa katikati ya barabara baada ya kupigwa risasi,Waafrika sijui tutazinduka lini kwa hii kitu mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
Ebu ona hii nayo jinsi watu walivyojificha kwenye mti kuokoa maisha yao na wengine wenye silaha wakiwa wanakimbia kuuawa.Mungu Ibariki Afrika,Mungu Ibariki Ivory Coast.
0 Comments