Baada ya wapenzi na mashabiki wa msanii wa anayekuja kwa kasi na kukubalika katika muziki wa BongoFlava kijana DIAMOND kukubaliana kwa pamoja wajumuike katika burudani hiyo pamoja jijini DEN HAAG nchini UHOLANZI,Ziara ya kufanya show nchini BELGIUM haitakuwepo baada ya makubaliano hayo.Akizungumza moja kwa moja ndani ya ofisi za Maganga One Blog,mmoja wa waandaji wa show hii alisema"Kwa kuwa wapenzi wote tumekubaliana tukafurahi kwa pamoja nchini Holland hakutakuwa na tatizo tukisitisha show ya Belgium kwa kipindi hiki"

Waandaaji wa show hiyo itakayofanyika Holland,wamesema kila kitu kipo safi kama kilivyopangwa,wanaomba tu washabiki waje kwa wingi kwani kutakuwa na burudani zaidi ya starehe.Kwa kuwakumbushia tu jinsi ya kufika anuani ni  
                         AT VAN
                         GIJNSTRAAT 11,
                         2288 GA RIJSIJK,
                         DEN HAAG,
  Watu wa kuwaulizia kila kitu kuhusiana na hii show ni Khatib mobile no-+31 681 812 2221 na bwana Kitanda kwa namba +31 684 0312 17.
Parking za magari zakutosha,Vinywaji na maakuli ndio usisemee.Vyombo vya musiki vitaongozwa na MA DJ'S Waliokwenda shule kwa shughuli za musiki.

Njoo uburudike na kuona vipaji vya MA' DJ watatu watakaotoana jasho kwa kukuburudisha wewe utakayeingia ukumbini,ma DJ hao ni
DJ KHATIB,
DJ KEE, NA DJ ALEIN.Kiiingilio ni sawa na bureee Euro 20 tu,Usisahau kumwambia na mwenzio tarehe 12/06/2011 ndani ya Den Haag patakuwa hapatoshi.