Mahakama moja nchini Ubeligiji imemuhukumu kijana mdogo mwenye umri wa miaka(26) kwenda jela mika 10 na miezi sita baada ya kupatikana na hatia ya kusababisha ajali barabarani.Kijana huyu aliyesababisha kifo cha aliyekuwa rafiki wake wa kike wakati anaendesha gari huku akiwa amelewa.Hakimu amemuhukumu huku akimkumbushia matukio mengine ya siku za nyuma aliyokuwa akiyafanya huku akiwa na pombe kichwani."Hii ni fundisho kwa wengine wote watakaofanya maovu kama yako" alimalizia hakimu huyo.