Nina msemo wangu huwa naupenda sana,kwamba "UKISHANGAA WATAKUSHANGAA" hapa mkoani kwangu,leo nimekuta bidada na mshirika wake wakiwasha mishumaa ambayo sikuweza kuihesabu kirahisi kwa jinsi ilivyokuwa mingi.Nilipotaka kuhoji kulikoni nilishindwa kwani bidada alikuwa bize sana nikaona nitampotezea dakika zake kwa maswali.
Ila nilihisi ni tukio la kumbukumbu ambalo hufanyika kila mara.kwani kila mmoja alikuwa busy na Camera yake na hata watu wa vituo maalumu vya Televisheni za kitaifa walikuwepo,mimi sikuacha kufyatua Flash yangu ili kuwaonyesha wanablog pengine kuna mmoja wetu anajua utaratibu huu ambao kwangu ulikuwa mgeni machoni mwangu.
Mimi yuleee mwenye sweta jekundu naendelea kukodoa macho tu bila mafanikio ya kumpata huyo bidada aliyechuchumaa chini akiendeleza kuwasha mishumaa niliyoshindwa kuihesabu.Jitihada za kutaka kujua nini maana ya kuwasha mishumaa mingi kiasi kile ziligonga mwamba,mpaka narudi kwenye ukurasa wetu mambo yalikuwa bilabila maana kama mnavyomuona bidada jinsi anavyowasha na mingine bado inamsubiri.



0 Comments