Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salam, Sulemani Kova, alisema wameamua kuweka mikakati hiyo kwa ajili ya kuondoa tatizo la foleni ambalo limekuwa kero kubwa kwa muda mrefu kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam na wageni wanaoingia.
"Kesho (leo) Jeshi la Polisi tutatangaza mikakati kabambe ambayo itasaidia kupunguza foleni ili kuinua uchumi wa wananchi, foleni ikiwa kubwa watu wakamaliza muda mwingi mabarabarani, kwa kiasi kikubwa inachangia uchumi kushuka", alisema Kamanda Kova.
Alisema anaamini mikakati watakayoianzisha itasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa foleni na hivyo kuwasaidia watu wengi kuwahi katika shuguli zao za kila siku.
Jiji la Dar es salam linakabiliwa na foleni kubwa za magari barabarani ambazo husababisha watu wengi kuchelewa ofisini na katika shughuli zao nyingine jambo ambalo limekuwa kero kubwa na kuzorotesha maendeleo.
CHANZO: NIPASHE


0 Comments