Rais mstaafu wa Zambia Frederick Chiluba(pichani) amefariki dunia nyumbani kwake baada ya kusumbuliwa na maradhi ya Moyo na Ini,msemaji wa aliyekuwa rais huyo bwana Emmanuel Mwamba alieleza.Rais huyo alifariki baada ya maumivu makali ya tumbo aliyokuwa akiyasikia.Alifariki ndani ya dakika tano tu baada ya maumivu hayo usiku wa manane nyumbani kwake alipokuwa akiishi.(maelezo zaidi nitawaletea baadae).