Kijana Nguyen pichani akiuonyesha mguu wake wenye kilo 80 na urefu usiopungua mita moja,anaomba msaada kwa msamaria mwema yoyote ili aweze kupata matibabu ya kuondosha uvimbe huo mguuni kwake.
Ndugu,jamaa,marafiki na watu mbalimbali wamekuwa wakijitokeza kumtembelea ndugu Nguyen kuhusiana na hali aliyonayo.Pichani kama unavyomuona jinsi mguu wake unavyompa taabu hata kusimama hawezi tena zaidi ya kukaa na kulala.
Akipata msaada wa kusafishwa na mama yake mzazi ambaye ni mtu mzima sasa mwennye miaka 61,Nguyen ameshindwa kupata matibabu mazuri kutokana na uwezo mdogo walionao yeye na familia yake.kwa habari zaidi unaweza kulitembelea gazeti la Nifahamishe.