Gavana wa jimbo la Sudan la Kordofan Kusini, anasema maisha yanarudi katika hali ya kawaida, baada ya ghasia za majuma kadha.
Gavana huyo, Ahmed Haroun, ambaye anasakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, alisema watu waliokimbia wanaanza kurudi.
Mashirika ya kutetea hali za kibinaadamu, yamewalaumu wakuu kuwa wamewalazimisha watu kurudi nyumbani, ingawa kulikuwa na mapambano makali baina ya jeshi la serikali, na watu hasa wa kabila la WaNubi.BBC