Viongozi wa Ulaya wamekubaliana kuipatia Ugiriki msaada mkubwa wa pili wa fedha ili kunusuru uchumi wake
.
Katika mkutano wao wa dharura uliofanyika Brussels, Ubelgiji viongozi hao wamekubaliana kutoa msaada wa zaidi ya dola bilioni 150.
Uamuzi huo umeungwa mkono na shirika la fedha duniani IMF.
Kwa mara ya kwanza, mashirika ya kukopesha ya kibinafsi, ikiwa ni pamoja na mabenki, yatahusishwa.
Mabenki na wawekezaji wa kibinafsi watatoa Euro bilioni 37 kama mchango wao.
Waziri mkuu wa Ugiriki, George Papandreou,amesema uamuzi huo utarahisisha maisha ya wagiriki.
"Sasa tunao mfumo ambao utawezesha Ugiriki kuweza kushughulikia madeni yake," Papandreou alisema.
Ilitarajiwa kuwa baada ya hatua ya kwanza ya kuisadia nchi hiyo, uchumi wake utaimarika kiasi kwamba wataweza kuomba mikopo ya kujisitiri kutoka mashirika ya fedha kwanzia mwaka ujao lakini hili huenda lisifanyike.
Kutokana na hali hii viongozi wa bara ulaya wanakubaliana kuwa juhudi zaidi zinahitajika kuisadia nchi hiyo.
Mpango ni kuwa Ugiriki utapata mkopo zaidi kutoka majirani wake na pesa zingine zitapatikana baada ya kuuzwa kwa baadhi ya mali za serikali.
Huku viongozi wa ulaya wakijiandaa kwa mkutano huo pia kumetolewa pendekezo kuwa benki za ulaya zililipia kiasi fulani cha kodi ambacho kitakumika kuisaidi ugiriki na nchi zingine zenye matatizo ya kiuchumi.
Tofauti na mkutano uliofanyika mwezi uliopita, safari hii soko la fedha nchini Uhusipania na Italia linakabiliwa na shinikizo kali tofauti na kipindi kilichopita.
Madeni ya nchi hizo ni makubwa zaidi ukilinganisha na yale ya Ugiriki, Ureno na Ireland, nchi ambazo zinapokea msaada kutoka umoja wa ulaya.
Kufuatia hali hii nchi wanachama wa umoja wa ulaya pia wamekubaliana kuongeza michango yao kwenye mfuko maalum wa kunusuru nchi zinazokabiliwa na matatizo ya kiuchumi.
0 Comments