Carlos Tevez(pichani juu) bado anataka kuihama Manchester City na kamwe "hana wasiwasi" kutokana na kuvunjika kwa harakati za kuhamia Corinthians, mwakilishi wake ameeleza.
Timu hiyo ya Brazil siku ya Jumatano ilijitoa kumuwania Tevez kwa kitita cha paundi milioni 40.
Kia Joorabchian ameiambia BBC: "Huyu ndiye Carlos Tevez tunayemzungumzia, mmoja ya wachezaji hodari duniani. Hatuna wasiwasi.
"Anataka kuondoka lakini bado ni mchezaji wa Manchester City na tutaendelea kuheshimu hilo."
Joorabchian amesema ana matumaini kutakuwa na vilabu vinavyomuhitaji mshambuliaji huyo, ambaye alisaini mkataba wa miaka mitano na Manchester City mwezi wa Julai 2009.
"Hebu na tusubiri na tuone nani mwengine atakayekuja kumuhitaji," alisema.
City walikuwa wamefikiriki wamefikia makubaliano na Corinthians kumuuza Tevez, lakini klabu hiyo yenye makao yake Sao Paulo iliamua kujitoa kwa sababu wasingeweza kukamilisha uhamisho kabla ya kufungwa kwa usajili wa wachezaji kutoka nje siku ya Alhamisi.
Tevez, ambaye alishawahi kuzichezea Manchester United na West Ham, amesema anataka kuondoka City ili awe na muda wa kutosha kuwa karibu na mabinti wake.
Aliwasilisha barua ya kutaka kuhama mwezi wa Desemba mwaka jana, kabla ya kuiondoa barua hiyo na akaisaidia timu yake kumaliza katika nafasi ya tatu ya msimamo wa Ligi.
0 Comments