Askari Polisi wa Bunge wakiwasindikiza wabunge wa CHADEMA Tundu Lissu (kulia) Mchungaji Peter Msigwa (kushoto) na Godbless Lema (wa pili kushoto) ili waondoke nje ya viwanja vya Bunge mara baada ya Naibu Spika Job Ndugai (hayupo pichani) kuwaamuru watoke ndani ya Bunge leo baada ya wabunge hao kuvunja kanuni za Bunge za kuongea bila ruhusa ya Naibu Spika. Wa pili kulia ni Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akiwasindikiza wabunge wenzake.
Naibu Spika Job Ndugai akiwaamuru wabunge wa CHADEMA Tundu Lissu, Mchungaji Peter Msigwa na Godbless Lema kutoka ndani ya Bunge leo mara baada ya wabunge hao kuvunja kanuni ya Bunge ya kuongea bila ruhusa ya Naibu Spika