Ufaransa imesema imekuwa na mawasiliano na ujumbe wa Muammar Gaddafi unaosema kiongozi huyo wa Libya "yuko tayari kuondoka."
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Alain Juppe(Pichani juu) aliiambia redio Ufaransa, " Uongozi wa Libya unatuma wajumbe kila sehemu, Uturuki, New York, Paris" wakitaka kujadili kuondoka kwa Kanali Gaddafi.
Lakini aliongeza mawasiliano hayo hayakuhusisha majadiliano.
Ufaransa ilikuwa mstari wa mbele katika kuanzisha mashambulio yanayoongozwa na majeshi ya umoja wa nchi za kujihami za Ulaya Nato, chini ya azimio la umoja wa mataifa la kulinda raia.
Bw Juppe aliiambia redio ya Ufaransa siku ya Jumanne: " Tunapata wajumbe wanaotuambia: ' Gaddafi yuko tayari kuondoka. Hebu tujadili.'
" Kuna mawasiliano lakini si kwamba majadiliano yameanza rasmi katika kipindi hichi."
Bw Juppe hakusema wajumbe hao ni akina nani.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa Bernard Valero alisema: " Hawa ni wajumbe wanaosema wanakuja kwa jina la Gaddafi. Kilicho muhimu ni kwamba tunawatumia ujumbe na kuwa karibu na washirika wetu kuhusiana na suala hili."
0 Comments