Bwana harusi mwenye kilemba cheupe na Hagar kichwani Jimmy kulia akiwa na mlezi wake ambaye ameiwakilisha familia ya bwana harusi katika shughuli nzima bwana Hija kushoto wakiingia ukumbini tayari kwa ndoa.
Bi harusi mwenye gauni refu la kijani katikati akiwa anasubiri hatua za mwishomwisho kuja kuulizwa kama amekubali kuolewa na bwana harusi.Bi harusi alikubali kwa kurudia mara 3 kama itikadi na taratibu za dini ya kiislam.kulia kwa bi harusi ni mama mzazi wa bi harusi.
Kwa Idhini ya wazazi bwana Yusuph kulia,ambaye ni mdogo wa bi harusi yeye ndiye aliyebeba madaraka ya kumuoza dada yake kwa bwana harusi Jimmy pichani kushoto.
Ndoa ilifungwa salama na hatimaye bwana Jimmy na bi Betty walihalalishwa kuwa mke na mume.
Watanzani,waburundi,wakenya,wakongo,waganda na mataifa mbalimbali walihudhulia sherehe hii,kwa kweli harusi ilifanya vilivyo.
Baada ya ndoa kufungwa sherehe ziliendelea za kumuaga bibi harusi usiku wake,bwana Jimmy na mkewe Betty walipendeza sana ukumbini hapo.Picha na madikodoki ya harusi hii yatakuja tena baadae.
0 Comments