WATU 11 wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine Drive , Dar es Salaam wakikabiliwa na shitaka la kuuza miili.
Waliofikishwa mahakamani ni Jasmin Mohamed (20) na Jenipha Julius (17) wakazi wa Mabibo , Mwajuma Hamis (19) mkazi wa Magomeni, Aliga Project (20) na Anjela Michael (19) wakazi wa Manzese.
Wengine waliofikishwa mahakamani hapo ni pamoja na Jeni Issa (19), Anna Keneth (19) na Jenipha Stanley (20) wakazi wa Tandale, Hidaya Rajabu (20) na Farida Hassan (20) wa Mbezi na Salome John (28) mkazi wa Sinza.
Mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo, William Mutaki, Mwendesha Mashitaka, Crispin Rwiza alidai Julai 13 mwaka huu washitakiwa hao walikutwa na askari aliyetajwa kwa jina moja, Julius, katika eneo la Kinondoni.
Alidai kuwa, huku wakitambua kuwa kufanya shughuli hiyo katika maeneo hayo ni kinyume na sheria ya makosa ya jinai kifungu kidogo cha 176 cha sheria No. 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Washitakiwa wote walikana kutenda kosa hilo na hivyo kurudishwa rumande hadi Julai 28 mwaka huu, baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana iliyowataka kuwa na wadhamini wawili watakaosaini dhamana ya Sh 10,000 kwa pamoja.
0 Comments