Magnus Malan, waziri wa ulinzi ambaye alikuwa mstari wa mbele kupinga utawala wa Waafrika nchini Afrika Kusini, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81.
Aliiongoza serikali ya wachache ya weupe katika mkakati wa "kuongoza harakati za vita bila huruma".
Hii ilihusisha kurusha mabomu nchi zilizo kusini mwa Afrika zilizounga mkono kufutwa kwa ubaguzi wa rangi na kutangaza hali ya dharura nchini humo kumaliza maandamano ya kuunga mkono demokrasia.
Alikuwa waziri wa kwanza kufikishwa mahakamani kwa ukatili enzi za ubaguzi wa rangi lakini aliachiwa mwaka 1996.
Jenerali Malan alikuwa na wadhifa wa waziri wa ulinzi kwa miaka 11 mpaka mwaka 1991, baada ya Rais FW de Klerk kumwondoa baada ya kushinikizwa na Nelson Mandela.
Bw Mandela alimshutumu Jenerali Malan kwa kuunda kikosi cha mauaji ili kuua wanaharakati wa ANC na kuleta mtafaruk Afrika Kusini kabla ya uchaguzi wa kidemokrasia.
Haya yalitokea mwaka 1994, huku ANC ikiwa imeshinda kwa kishindo na Bw Mandela kuwa Rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini.
Katika miaka ya 80, Jenerali Malan aliidhinisha ghasia dhidi ya wanaopigana kupinga ubaguzi wa rangi Angola, Lesotho, Msumbiji, Zambia na Zimbabwe.
Alifikishwa mahakamani kwa kuhusishwa na mauaji ya watu 13 kwenye jimbo la KwaZulu-Natal mwaka 1987 na kutoa mafunzo ya kijeshi kinyume cha sheria kwa wanaopinga watu weusi wa ANC.
Alitangaza kesi hiyo "siku ya kiza" kwa demokrasia inayokua Afrika Kusini, wakati wanaharakati wa ANC walilaumu kuachiwa kwake na jaji aliyekuwa aikiskiliza kesi hiyo enzi za ubaguzi wa rangi.
Pia aliongoza mazungumzo yaliyosaidia katika kupata uhuru wa Namibia mwaka 1990, ikisitisha hadhi yake kama koloni la Afrika Kusini.
Familia yake imesema amekufa kwa amani nyumbani kwake na ameacha mjane, watoto watatu na wajukuu tisa.
0 Comments