Hili ni duka la raia wa Morocco nchini Holland,nimezunguka na kuona raia hawa wamefanikiwa kuwekeza nchini Holland kwa sana tu,maduka mengi na migahawa mingi ni ya raia hawa wa Morocco,ikiwa na sisi tutajaribu kuwaleta wawekezaji kama hawa nchini kwetu nafikiri tutapiga hatua kiuchumi.
Hapa ni Mega stores jijini Den Haag,kuna kila aina ya maduka na panavutia sana,nilipozunguka na kukagua vitu fulanifulani ambavyo kule kwetu hakuna vya uhakika,moja niligundua ulinzi uliopo pale ni wa uhakika na tofauti na kwetu ukiacha gari yako uenda ukakata umeibiwa kabisa.
Migahawa yao ni mizuri,misafi na huduma zao ni za haraka kwa kweli nimeinjoi,naendelea kujifunza zaidi.
Nchi mbalimbali ukifika kama hujui lugha ujue hali tete imekufika,ila nchini Holland wao tofauti kidogo juu ya suala zima la lugha,wana vyuo vingi sana ambavyo ulazimisha wageni kujifunza lugha ya kwao.sijui na sisi lugha ya Swahili tunaitangazaje ndani na nje ya nchi yetu.Pichani ni moja ya chuo cha kufundisha lugha kilichopo Den Haag.
Nilifanikiwa kutembelea chuo alichosoma shemeji yangu,hiki ni chuo ni kikubwa na kinafundisha mambo mengi sana juu ya masuala ya kazi.kwa kweli nilifundishwa mengi sana juu ya kila swali nililokuwa nikiuliza.wafanyakazi wa pale ni watu hodari sana,wakarimu na wanajua nini wanafanya wawapo kazini.
Serikali za wenzetu zinajali sana miji yao,pichani namuona mtumishi wa serikali akipaka rangi nguzo ya taa barabarani,kwa kweli inapendeza sana kuona kodi za wananchi zinatumika ipasavyo.
Angali hii picha vizuri,kushoto kabisa sisi watembea kwa miguu,barabara inayofuata ni ya waendesha baiskeli kisha tunamalizia barabara ya gari,hii inasaidia sana kuepusha ajali za barabarani kwani kila mmoja amepewa nafasi kubwa sana kiusalama tofauti na na njia zetu nyumbani,siwafundishi kazi wahusika ila itabidi tujifunze kwa vitendo.
Tofauti na nyumbani nimeshazoea nikienda kununua vifaa vya ujenzi na umeme navikuta nje ya duka,ila nimezungukia maduka haya ya vifaa vya ujenzi na umeme hapa Holland kiukweli inapendeza sana kuona watu wanaheshimu kazi zao kama unavyoona moja ya duka kubwa kabisa likiwa limepangwa kila vifaa sehemu husika na ni ndani sio nje ya duka.
Nyumbani Garden (sehemu za mapumziko) zimekuwa ndio Garage za kutengenezea magari mabovu,tofauti na wenzetu ambao sehemu kama hizi zinaheshimika sana na kweli kama unavyoziona watu wamejipumzisha na panavutia kwa usafi.watoto wanacheza na wazazi wapo pembezoni wakiwaangaalia huku wakipata upepo mwanana.
Ebu ona viwanja vya wazi jinsi serikali inavyovithamini,vimejengwa maalumu kwa ajili ya watoto na watu kupumzika,sio kwetu wababe wameuziwa
Hapo napo watoto wanaruka juu ya kamba maalumu zilizowekewa ulinzi wa kutoumia kwao.
Nimevutiwa sana na sehemu za mapumziko,naomba sana n serikali zetu ziliangalie upya suala hili la maeneo ya wazi kufanywa kama hivi.
Vivuko kama hivi ambavyo vinatushinda kabisa kuvitengeneza,wenzetu kiukweli serikali zao zinawajali na kujali kodi za wananchi wake.
Barabara na alama za barabarani,taa za barabarani yani kila kimoja kinafanya kazi na kufuatwa kama taratibu zilivyopangwa,ukijaribu kukiuka taratibu na sheria hizi kiukweli utajikuta mahala pabaya,serikali za wenzetu hazina rushwa,hazina kuonea haya,ukikiuka taratibu mahakama inachukua mkondo wake.Naendelea kujifunza nipo mitaani bado,nitawapa mengine zaidi baadae.
2 Comments